Monday 18 July 2016

TOKA KWA ISMAIL M SUMAJL

SAMAHANI NI YA SIKU ZOTE SIO MPAKA UFUMANIWE.


Neno Msamaha halipo kwa ajili ya makosa makubwa peke yake, kama ulikuwa hujui basi leo ujue hata makosa madogo yanahitaji kuomba msamaha,

Hasa wanaume wengi huwa hawaoni umuhimu wa kuomba msamaha, kwa kuona walichokifanya ni kidogo tena wakihusisha wao ndio wakuu wa kaya, Wanawake wao hutumia Neno Si yaishe tu kwanini unapenda kuyakuza, yaani hapo ndio kaomba msamaha,.
Sasa kuanzia leo Uweke dhamira ya kuwa unaomba msamaha na ukijiona Samahani zitakuwa nyingi basi uanze kupunguza makosa yako, Mfano mwanaume asubuhi wakati unaenda kazini uliahidi ukirudi utamletea mkeo chipsi za free point (chipsi maarufu kwa sasa kwa wakazi wa dodoma mjini), unafika njiani wakati unarudi jioni kwa bahati mbaya umesahau na unaamua kununua za njiani hapo, kufika nyumbani ubavu wako unaanza kula na kugundua sio zenyewe, cha msingi hapa mweleze ukweli kisha muombe samahani, nawe unaeombwa pokea samahani hiyo, sio ndio uanze kelele mpaka jirani wasikie kwa maana mwanaume kumvumilia mwanamke mwenye kelele ni sawa na garimoshi kuanzisha safari za Dar to Unguja,


Anza kuomba samahani leo isingoje kesho, kwani samahani ni ishara ya upendo, Umesahau kumletea Apple muombe Samahani usisubiri Kuja kuomba Samahani Mpaka AKIKUFUMANIA.
Mwandishi wa Post hii ni Msela tu fulani asiyejua hata radha ya ndoa ila amejitolea kuwasaidia mlieingia ndani ya ndoa na kusahau majukumu yenu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!