Sunday 3 July 2016

Tisa waliokufa ajalini Moro watambuliwa



Morogoro. Majina ya marehemu tisa kati ya 11 yametambulika kutokana na ajali ya magari matatu iliyosababisha vifo vya watu hao.



Tayari majeruhi 43 wa ajali iliyotokea Dakawa wilayani Kilosa wamehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.
Majeruhi hao wamehamishiwa katika hospitali hiyo kutokana na kuumia vibaya, huku miili ya marehemu watatu ikiwa haijatambulika majina wala wanakotoka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema kutokana na ajali hiyo jeshi hilo linamsaka dereva wa lori lililokuwa limebeba kontena kwa kusababisha ajali na vifo vya watu watato na baadaye kusababisha ajali ya watu wengine.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!