Saturday 16 July 2016

Tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo



Mawe ya mfuko wa nyongo ni mkusanyiko wa chembe ndogondogo ngumu katika mfuko huo ambao ni kiungo kinachohifadhi nyongo ambayo ni kimeng’enya cha chakula kinachozalishwa kwenye ini.



Mawe ya mfuko wa nyongo hutofautiana ukubwa. Mengine huweza kuwa madogo kama punje ya mchanga lakini pia kuna makubwa kama mbegu ndogo za badhi ya matunda Baadhi ya watu hupata jiwe moja kwenye mfuko wa nyongo na wengine mengi kwa wakati mmoja.

Lakini pia wapo ambao huwa na dalili kutokana na kuwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo huhitaji upasuaji wakati wale wenye mawe yasiyosababisha dalili zozote huishi bila kuhitaji matibabu yoyote.
Chanzo cha mawe kwenye nyongo?
Mawe ya mfuko wa nyongo hutokea pale ambapo vitu vilivyomo kwenye nyongo hugandana na kuwa vigumu hali ambayo husababisha kutengenezeka kwa jiwe/mawe. Katika hali ya kawaida nyongo ina vitu kama lehemu (cholesterol), ‘bilirubin’pamoja na madini ya chumvi ya kalisi.

Sababu za mawe hayo ni kiwango kikubwa cha helemu, nyongo kwa kawaida huwa na kemikali maalum ya kutosha kwa ajili ya kuyeyusha helemu ambayo hutolewa mwilini na ini .
Iwapo ini litatoa kiwango kikubwa ya helemu kuliko ambavyo nyongo inaweza kuyeyusha kiasi kilichozidi hugandana na kutengeneza chembe ngumu ambazo baadaye huwa mawe ya kwenye mfuko wa nyongo.
Kiwango kikubwa cha ‘bilirubin’
Bilirubin ni kemikali ambayo hutengenezwa pale mwili unapovunjavunja chembe hai nyekundu kutokana na sababu mbalimbali. Zipo hali mbalimbali ambazo hufanya ini kuzalisha kiwango kikubwa cha bilirubin. Hizi ni pamoja na tatizo la kuharibika kwa ini tatizo lijulikanalo kama ‘liver cirrhosis’.

Maambukizi katika mrija wa kupitisha nyongo pamoja na matatizo kadhaa ya damu. Kiwango hiki cha ‘bilirubin’ kilichozidi kwenye mwili ndicho hugeuka na kuwa chanzo cha mawe kwenye mfuko wa nyongo.
Hitilafu kwenye kumwaga nyongo
Iwapo mfuko wa nyongo haumwagi nyongo ipasavyo tumboni nyongo iliyopo kwenye mfuko inapobaki kwa muda huendelea kuwa katika hali ya ukali au (concentrated) na kuchangia kutokea kwa mawe kwenye mfuko.
Aina za mawe ya nyongo

Zipo aina mbalimbali za mawe kwenye mfuko wa nyongo kutegemeana na chanzo chake. Aina hizi ni pamoja na;mawe ya helemu ‘cholesterol gallstones’:
Hii ndo aina kubwa zaidi ya mawe ya mfuko wa nyongo ambayo huwapata watu wengi zaidi.Mawe haya huwa na rangi ya njano haya yana kiwango kikubwa cha lehemu japo huweza kuwa na chembechembe nyingine pia.
‘Pigment gallstones’
Mawe haya yana rangi ya ugoro au nyeusi na hutokea pale ambapo nyongo inakuwa na kiwango kikubwa cha kemikali aina ya ‘bilirubin’.

Dalili za mawe ya mfuko wa nyongo
Mawe katika mfuko wa nyongo yanaweza kuwapo bila mhusika kupata dallili au ishara yoyote. Hata hivyo idadi kubwa ya watu wenye mawe ya mfuko wa nyongo hawapati dalili zozote, hali hii huitwa mawe ya nyongo yaliyotulia ‘silent’ gallstones’.

Katika hali hii daktari anawezakugundua mawe haya kwa njia ya mionzi kama X-ray au pale mtu anapofanyiwa upasuaji wa tumbo. Iwapo jiwe litaziba mrija unaopitisha nyongo basi dalili huanza kuonekana haraka.
Dalili hizo ni pamoja na maumivu ambayo ni ya ghafla sehemu ya juu ya tumbo upande wa kulia. Maumivu sehemu ya mgongo au bega la upande wa kulia.Maumivu katikati ya mifupa ya mabega ya mgongoni ‘shoulder blades’.
Maumivu makali na makali sehemu ya kati ya tumbo chini ya mfupa wa kati ya kifua.

Katika hali ya kawaida na ya kihalisia mwili hutengeneza lehemu , hata hivyo mwili huweza pia kupata helemu kutokana na aina ya chakula mtu anachotumia. Sababu nyingi zinazomuweka mtu katika hatari ya kupata mawe ya mfuko wa nyongo husababishwa na aina ya chakula kinacholiwa.
Hii ni pamoja na; kuwa na uzito kupita kiasi, ulaji wa vyakula chenye kiwango kikubwa cha mafuta au helemu, kupungua uzito kwa ghafla ndani ya kipindi kifupi, pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari.
Aidha, hali nyingine ambazo humuweka mtu katika hatari ya kupata mawe ya mfuko wa nyongo ni pamoja na ujauzito, kuwa na familia yenye historia ya tatizo la mawe ya mfuko wa nyongo, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha helemu, umri mkubwa kuwa na tatizo la kuharibika kwa ini pamoja na matumizi ya dawa zenye kiwango kikubwa cha homoni aina ya ‘oestrogen’.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!