Kutokuwa na hela sio kuzuri kabisa.Lakini kutokuwa na NDOTO ndio Kubaya zaidi.Umewahi kuwa na NDOTO tena ndoto kubwa lakini hujui uanzie wapi kuifanyia kazi.Huna hela maana ndoto yenyewe inataka pesa kuweza kuifanyia kazi.
Maisha ni magumu na wakati mwingine fursa zinakupita.Kwani wewe nani?hapa mjini nani anakujua?huna pakuanzia..huna connection.Katika kutapa tapa kutafuta connection bado utafungiwa milango pia na mawazo yako yakaibiwa vile vile na wenye pesa wakazifanyia kazi.
Utapambana sana utasukuma haswaa lakini wapiii...na mwisho matumaini ya kutimiza ndoto zako yatakufa.
Utapambana sana utasukuma haswaa lakini wapiii...na mwisho matumaini ya kutimiza ndoto zako yatakufa.
Utadharaulika hata kuchekwa mwisho uachilie ndoto yako ukihisi haiwezekani.Utafanya kazi Hata zisizo za ndoto yako ili upate kula na pengine Hata kula iwe taabu...inatokea sanaa.
NIKWAMBIE Hata iweje endelea kubeba maono yako.Lolote litakalo kutokea ukapata ugumu kutimiza ndoto yako usiachilie..usikate tamaa.Hata wakikuvunja moyo wewe endelea kuamini...ipo siku.
Hakuna anaejua uwezo ulionao ila wewe mwenyewe.Ipo siku struggle zako zitakuwa hadithi nzuri ya wengine kujifunza wakati ukiishi ndoto yako!
No comments:
Post a Comment