Kijana Huyu alipata kipigo baada ya kudai nyongeza ya Mshahara ikiwa na wenzake mgodini
Nimefika Mgodi wa Nyamhuna unaodaiwa kuwa raia wa china ambao ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo wakishirikiana na watanzania walimtesa kinyama na kumjeruhi mmoja wa mtanzania mwenzetu aliyekuwa akifanya kazi katika mgodi huo uliopo Katoro-Geita.
Imenilazimu kufika gereza la Geita kukutana na kijana huyo ambae yupo hai tofauti na taarifa za awali kuwa alifariki.Baada ya kujiridhisha kuanzia mavazi,majeraha,picha,sura na umbo lake kuwa ndiye kijana aliyeteswa vibaya na picha zake kusambaa mitandaoni na vyombo mbalimbali vya habari,niliamua kwenda naye hadi mgodini lilipofanyika tukio hilo la kinyama,aliwatambua wahusika ambao NI KWELI WALIFANYA TUKIO HILO LA KINYAMA NA LISILOKUBALIKI HAPA NCHINI.
Hivyo walioshiriki tukio hilo tumeshawashikilia kupitia jeshi la polisi tayari kwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Nalaani tukio hilo vikali sana,serikali hii ipo tayari kushirikiana na kila mmoja rai mwema kutoa taarifa popote pale za matukio au viashiria viovu na vinavyohatarisha usalama wetu.
"Usalama wetu,jukumu letu sote"
Nalaani tukio hilo vikali sana,serikali hii ipo tayari kushirikiana na kila mmoja rai mwema kutoa taarifa popote pale za matukio au viashiria viovu na vinavyohatarisha usalama wetu.
"Usalama wetu,jukumu letu sote"
1 comment:
Tabia ya kuwalamba miguu wageni(non Tanzanian) hiyo ndio matokeo yake.nimejiuliza sn mchina anapata wapi hii jeuri ya kumjeruhi mfanyakazi wake namna hiyo. mungu wangu nchi km Norway Mtanzania angefanya hivo,hakuna maongezi ni kurudishwa nyumbani . NITASHANGAA SN KM HUYO MCHINA ATAENDELEA KUISHI
TANZANIA. Binafsi naomba serikali imnyang'anye uraia huyo mchina.Watanzania wenzako tuachane na ule ujinga wa kuwanyenyekea/kuwasujudia/kuwaabudu wageni na kuwadharau watanzania wenzetu.Sasa mtanzania akidharauliwa Tz unategemea akaheshimiwe wapi?Ulaya? Marekani? Heshima ni bidhaa adimu kwa mtanzania aliyeoko nje nchi yake, watu wanavumilia tu.MTANZANIA KWANZA NDANI YA TANZANIA YAKE.
Post a Comment