Monday 18 July 2016

Mwendokasi sasa kujengwa hadi Mkuranga






BAADA ya kuanza kufanya kazi kwa awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam, serikali imesema awamu ya pili inatarajiwa kujengwa kutoka Dar es Salaam hadi Vikindi mkoani PwaniHayo yalisemwa juzi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokuwa akizungumza na wakazi wa vijiji vya Mkiu, Njopeka na Lukhanga, alipofanya ziara katika kiwanda cha kutengeneza vigae vya sakafuni na ukutani, kilichojengwa na wawekezaji kutoka China.


Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kiwanda hicho, ambacho kinatarajia kukamilika ujenzi na kuanza kazi Septemba, mwaka huu, aliwataka watu kutumia fursa hiyo kujenga hoteli, maduka ya kisasa kutokana na eneo hilo kuchukuliwa na watu wengi ambao wameomba kuwekeza.
Alisema kutoka na Wilaya ya Mkuranga kuwa na ongezeko kubwa la watu na wengi wanaonyesha kwenda kuwekeza na hali hiyo kufanya hata kuwapo kwa foleni kutoka Dar es Salaam hadi Mkuranga, hiyo serikali imejipanga kuanzisha kwa usafiri wa mabasi ya mwendo kasi.
"Mradi wa awamu ya pili unatarajia kuanza jijini Dar es Salaam hadi Vikindu mkoani Pwani, ili kuwawezesha wananchi waache kukaa katika foleni kwa muda mrefu,” alisema,
Aliongeza kuwa Mkuranga imepanuka na kuchukua nafasi ya Dar es Salaam, hivyo kuna haja ya kuboresha barabara ili kurahisha mawasiliano baina ya maeneo hayo.
"Hii ni baraka kwenu. Kuna kampuni sita zinataka kuwekeza hapa, sasa mjenge hoteli, nyumba za kulala wageni na maduka ya kisasa,” alisema Majaliwa.
Wakati wa kuanza kwa usafiri wa mabasi ya mwendo kasi hivi karibuni, serikali ilisema awamu inayofuata ni kujenga barabara kutoka katikati ya jiji hadi Mbagala na Gongo la Mboto ili kupanua wigo wa miundombinu hiyo.
Akizungumzia kuhusu uwekezaji, alisema serikali imedhamiria kujenga viwanda ili kuongeza uchumi wa nchi.
Alisema viwanda vikijengwa hali hiyo itasaidia kuondoa uchumi wa chini na kuwapo kwa uchumi wa kati na kwamba panapokuwapo na viwanda, kunasaidia hata vifaa kuwa bei ya chini.
Wakati huo huo, Majaliwa aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho pamoja na ubalozi wake kutoa Sh. milioni 40 kwa ajili ya ununuzi wa madawati.
katika mchango huo, kiwanda hicho kimechangia Sh. milioni 20 huku ubalozi wa China nchini, ukichangia kiasi kama hicho kwa ajili ya kufanikisha upatikanaji wa madawati kwa mkoa wa Pwani.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!