Monday 4 July 2016

MUFTI AKEMEA UBAGUZI WA DINI NA UKABILA.


SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mufti Alhaji Abubakari Zubery

SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mufti Alhaji Abubakari Zubery, amewataka Watanzania kudumisha amani na utulivu bila ya kujali tofauti ya dini, rangi au kabila



Amesema kwak ufanya hivyo Watanzania watajiepusha na migogoro inayotokana na tofauti mbalimbali.


Mufti alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam, wakati wa chakula cha futari kilichoandaliwa na Kampuni ya Vifurushi ya City Delivery Cervices (CDS).
Zubery alisema jukumu la kulinda amani ni la kila Mtanzania kulingana na nafasi yake na wala si la kuwaachia vyombo vya ulinzi na usalama peke yake.
Alisema katika kipindi cha kumalizia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Waislam wameonyesha umoja na mshikamano, hivyo wanapaswa kuendeleza hali hiyo hata siku za kawaida, ili kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika kuilinda amani na kuleta maendeleo.
“Amani ni jukumu la kila mmoja wetu, hivyo tunapaswa kushirikiana na kuhakikikisha tunailinda na kuishi pamoja kama ndugu bila kujali tofauti ya rangi, dini au kabila,” alisema Mufti Zubery.
Aliongeza kuwa nchi zote zilizopata maendeleo ziliwekeza katika ulinzi wa amani, hivyo wananchi wa Tanzania wanapaswa kujifunza katika nchi hizo ili kuongeza upendo na mshikamano.
“Watanzania tumepata bahati ya kuwa na amani, umoja na mshikamano hadi sasa. Hii inatokana na uvumilivu wa wananchi wote bila kujali tofauti zilizopo, hivyo basi tunapaswa kuendeleza hapa tulipofikia ili tuweze kuwa mfano wa kuigwa,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CDS, Masoud Wang’anyi, alisema bila kuwepo kwa amani, kazi za ujenzi wa taifa hazitafanyika, jambo ambalo linaweza kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
“Tunafanya kazi kwa sababu kuna amani na utulivu, bila hivyo hakuna kitakachofanika. Kutokana na hali hiyo, tunapaswa kujifunza kwenye nchi ambazo tayari zimeingia kwenye migogoro ili tuweze kujiepusha,” alisema Wang’anyi.
Aliongeza kampuni yake inafanya kazi na taasisi za serikali, dini na watu binafsi na hali hiyo inatokana na mshikamano uliopo. Kutokana na hali hiyo, alisema wanapaswa kuongeza mshikamano ili kuhakikisha nchi inapata maendeleo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!