Mafanikio hayo ni matokeo ya mradi wa majaribio uliofanywa na Taasisi ya Afya Ifakara kwa miaka nane, kati ya 2007 hadi mwaka jana.
Mkuu wa Utafiti wa Huduma za Afya kwa Jamii wa taasisi hiyo, Dk. Fatma Manzi alisema mradi huo uliofadhiliwa na taasisi ya Doris Duke Charitable ya Marekani pamoja na Comic Relief ya Uingereza, ulilenga kupunguza vifo hivyo.
Alisema huduma hiyo ililenga kutoa huduma bora uzazi na kuhakikisha kina mama wanajifungulia katika vituo vya afya.
“Matokeo na mafanikio ya kwanza namna tulivyoweza kuuunganisha jamii na huduma za afya kupitia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii (WAJA) ikiwamo kuandaa sera kwa huduma ya afya katika utekelezaji wa huduma hizo,” alisema Dk. Manzi.
Alisema mradi huo pia uliweza kutoa mafunzo kwa wahudumu hao kwa muda wa miezi tisa, ikiwamo kuwapatia vifaa tiba vya kutolea huduma katika jamii.
Naye Mhudumu wa ngazi ya Jamii, Hamisi Mahangae alisema walipokuwa wakitoa huduma katika jamii changamoto kubwa ilikuwa kwa jamii kutokana na baadhi yao kutochukua hatua za haraka za kumpeleka mtoto hosptali kutokana na ukosefu wa fedha.
“Changamoto ni ukosefu wa fedha, wanajamii wengi wanakosa fedha ya usafiri ili kumfikisha mtoto wake haraka hospitalini ili akapatiwe huduma,” alisema Mahangae.
NIPASHE.

No comments:
Post a Comment