Wednesday 13 July 2016

Mapya yaibuka utafiti chimbuko la binadamu bonde la Oldupai


Taarifa ya kugundulika kwa masalia hayo ya kale, ilitolewa na mhifadhi wa paleontolojia (masalia ya kale), Dk. Agness Gidna kutoka Makumbusho ya Taifa, baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, kutangaza ugunduzi mpya wa nyazo za zamadamu, Julai 8, mwaka huu, katika eneo la Laetoli lililoko ndani ya NCAA.



Nyayo hizo zamadamu zinadaiwa kuishi miaka milioni 3.7 iliyopita.
“Katika utafiti wetu tumepata masalia hayo ya binadamu wa kale…ni meno ya binadamu aliyekuwa anakula vyakula vigumu,” alisema Dk. Gidna.
Hata hivyo, alisema sehemu ya kichwa cha mtoto kiligunduliwa miaka mitatu iliyopita na wameihifadhi Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Alisema utafiti wao umeonyesha kwamba mtoto huyo alifariki siku mbili au tatu baada ya kuzaliwa miaka milioni mbili iliyopita.
Alisema bonde la Oldupai lililopo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ni sehemu yenye historia ya pekee ya chimbuko la binadamu na kwamba hakuna sehemu yoyote duniani inayoelelezea historia ya binadamu kama ilivyo hapo.
Utafiti huo ni sehemu ya mradi wa ulioandaliwa na NCAA chini ya Mhandisi Joshua Mwankunda na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) iliyotoa Euro milioni 1.8 karibu sawa na Sh bilioni 4.3) kwa ajili ya shughuli za kuhifadhi zana za kale na asili ya chimbuko la binadamu katika bonde la Oldupai.
Chini ya mradi huo, ujenzi wa makumbusho ya kisasa kwa ajili ya kuhifadhi masalia hayo yanaendelea kujengwa hapo Oldupai.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!