Tuesday 12 July 2016

MAPISHI YA LEO: KAMBA WA NAZI NA SPINACH


VIPIMO A.
🔹Kamba (shrimp) 12-14 kubwa
🔹Maji ya limao kjk 1½ chakula
🔹Pilipili ya cayenne 1/2 kijiko chai
🔹Chumvi na pilipili manga kiasi
VIPIMO B.

🔹Mafuta ya kula vjk 2 chakula
🔹Kitunguu maji kilicho katwa katwa 1
🔹Hoho nyekundo ilokatwa vibox
🔹Kitunguu saumu kilichosagwa vjk 2 chai
🔹Tangawizi ilosagwa vjk 2 chai
🔹Giligilani ya unga kjk 1½ chai
🔹Binzari ¾ kjk chai
🔹Manjano ¼ kjk+ ⅛ kjk chai
🔹Nyanya zilizokatwa katwa pamoja na mchuzi wake vikombe 2
🔹Sukari kjk 1 chai
🔹Tui la nazi zito vikombe 2
🔹Chumvi na pilipili manga kiasi
🔹Spinach mkono 1
JINSI YA KUPIKA
1. Katika bakuli tia mahitaji yote A changanya vzr. Kisha acha viungo viingie vzr kwa muda wa dk 15.
2. Tia sufuria na mafuta jikoni, tia vitunguu maji na hoho nyekundu, pika kwa dk 4 hadi ziwe laini.
3. Tia kitunguu saumu kaanga kwa dk 1 kisha tia tangawizi,giligilani,binzari pamoja na manjano kaanga kwa dk 1.
4. Tia nyanya pamoja na sukari koroga vzr acha itokote kwa dk 15.
5. Tia tui la nazi kisha koroga na acha utokote kwa dk 10. Onja kisha tia chumvi na pilipili.
6. Tia spinach na kamba pamoja na sauce yake kisha acha itokote hadi kamba waive.
7. Kula mchuzi wako kwa wali.

special thanks to Mapishi mix...

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!