Friday 15 July 2016

ISIS waua 75 Ufaransa

Shughuli za uokoaji zikiendelea mjini Nice

Paris. Zaidi ya watu 75 wameripotiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Nice kaskazini mwa Ufaransa.


Lori lililokuwa likienda mwendo kasi lilijiingiza katika mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiangalia maonesho ya fataki kuadhimisha siku ya kitaifa ya Bastille, ambayo huja na shamra shamra kila mwaka.


Hata hivyopolisi walifanikiwa kumuua dereva wa lori hilo baada ya kutokea majibzano ya risasi yaliyochukua muda mrefu kwenye tukio hilo.
Kundi la ISIS limekiri kuhusika na shambulio hilo lililotokea nchini humo wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Bastille.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!