GEREZA la Kilimo la Songwe lililoko mjini Mbeya, litahamishwa eneo lililopo sasa hivi ili kupisha uchimbaji wa madini ya aina ya Niobium yaliyopo chini ya gereza hilo. Taarifa hiyo imetolewa na mwakilishi wa kampuni ya Panda Hill yenye dhamana ya kuchimba madini hayo.
Akizungumza mwakilishi wa kampuni hiyo alisema kuwa kampuni hiyo imejipanga kutoa kiasi cha TZS bilioni 400 ili kuhamisha gereza hilo pamoja na nyumba za wafanyakazi ili zoezi la uchimbaji lianze mara moja.
Katika uchimbaji huo wa madini takribani watanzania 467 wanatarajiwa kuajiriwa mara tu zoezi la uchimbaji utakapoanza hapo mwakani. Uchimbaji wa madini hayo unatarajiwa kudumu kwa muda wa maika 30.
Aidha, imeelezwa kuwa eneo hilo ni la nne kugunduliwa kwa madini hayo duniani huku likiwa ni eneo pekee lenye madini hayo barani Afrika. Wakizungumza viongozi wa mkoa wa Mbeya walisema kuwa serikali inatarajiwa kunufaika kupitia jaira, kodi, alisema Mkuu wa Mkoa Amos Makalla.
No comments:
Post a Comment