Saturday 9 July 2016

DEREVA WA CITY BOYS KORTIN



Singida. Dereva wa basi la City Boys, Jeremia Sempungwe (33) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida akikabiliwa na makosa 30 ya kusababisha vifo vya abiria 30 bila kukusudia.

Awali, Hakimu wa Mahakama hiyo, Joyce Minde alimweleza mshtakiwa kuwa atasomewa makosa yake yote lakini hataruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikilza kesi za mauaji.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali mkoani Singida, Zakaria Ndaskoi alidai kuwa Julai 2, mwaka huu Sempungwe akiendesha basi kutokea Dar es Salaam kuelekea Kahama, basi hilo liligongana uso kwa uso na basi lingine la kampuni ya City Boys na kusababisha vifo vya abiria 30 bila kukusudia na majeruhi 54

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!