Thursday, 28 July 2016

ALIYEPIGA PICHA YA MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI AFARIKI DUNIA

1

MPIGAPICHA mkongwe nchini wa gazeti la TanzaniaDaima, Joseph Senga, ni kati ya walioshuhudia tukio la kuzingirwa, kuteswa hadi kuuawa kwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel 10 Daudi Mwangosi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.

Habari za kusikitisha ni kuwa mpiga picha huyo mkongwe Joseph Senga amefariki Dunia nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Senga amefariki ikiwa ni siku moja tu tangu hukumu ya kesi ya Daudi Mwangosi kutolewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Iringa ambapo mshtakiwa amehukumiwa kwenda jela miaka 15 kwa kuua bila kukusudia.
Mwaka 2012 akiwa mfanyakazi katika kampuni ya Free Mdeia inayochapicha gazeti la TanzaniaDaima, Senga alikuwa ndiye mpiga picha bora wa mwaka kwa kupiga picha ya kuuawa kwa Daudi Mwangosi.
SWAHILI TIMES BLOG.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!