Sunday, 19 June 2016

Wenye ualbino Afrika wacharukia ukatili dhidi yao


WASHIRIKI wa kongamano la watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) barani Afrika linaloendelea jijini Dar es Salaam wameweka malengo ya pamoja ya kupaza sauti zao kupinga ukatili dhidi yao yakiwemo mauaji yanayofanywa kwa imani potofu za ushirikina.


Akizungumza jana kwenye kongamano hilo, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Albino nchini Afrika Kusini, Kamishna Nomasonto- Grace Mazipuko alisema kongamano hilo limewaunganisha ili kuja na nguvu ya pamoja kupinga ukatili na vitendo vya unyanyasaji dhidi yao.
Alisema serikali za nchi za Afrika zinapaswa kuwa na lugha moja kupinga ukatili unaofanywa kwa watu wake ambao wana ualbino kwa sababu wana haki ya kuishi sawa na watu wengine wasio na ualbino.
Kamishna Mazipuko alisema bado kuna changamoto ya kupewa nafasi kwa watu wenye ulemavu wenye sifa barani Afrika na kutoa mfano kuwa nchini Afrika Kusini ni asilimia mbili tu ya albino ndio waliopata ajira.
Alisema makundi ya wanawake na wasichana wenye ualbino bado yana changamoto, hivyo kuna haja ya kuwa na sauti moja kuhakikisha fursa mbalimbali zinatolewa pia kwa makundi hayo ili kuionesha jamii kuwa nao ni watu na wana uwezo wa kufanya kazi kama wale wasio na ualbino.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu Dk Abdallah Possi alisema serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili wadau na taasisi zinazoshughulikia watu wenye ulemavu, wafanye kazi zao kwa wepesi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!