Friday, 24 June 2016

Waziri Mkuu Cameron kujiuzulu baada ya Uingereza kujitoa EU



Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron.
London, Uingereza. Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ametangaza kuachia ngazi kwenye wadhifa wake muda mchache baada ya kura za maoni kuonyesha kuwa upande unaotaka kujitenga na Umoja wa Ulaya (EU) kushinda.


Matokeo ya kura za maoni iliyofanyika jana asilimia 52 ya Waingereza wamepiga kura ya kujitoa katika umoja huo, huku asilimia 48 wakitaka kubaki.
Cameron amesema amevunjwa moyo na matokeo hayo hivyo hana chagua jingine zaidi ya kuondoka madarakani. Amesema ataachia wadhifa huo Oktoba mwaka huu.
“Nilipigana ili tuendelee kusalia kwenye Umoja wa Ulaya lakini wananchi wa Uingereza wamefanya uamuzi wao hivyo binafsi napenda kuutaarifu umma kuwa nitaondoka madarakani baadaye mwaka huu,” amesema kiongozi huyo.
Baada ya matokeo hayo, Paundi ya Uingereza imeanguka ghafla dhidi ya dola ya Marekani chini ya dola 1.35; anguko ambalo linatajwa kua halijapata kutokea tangu mwaka 1985.
Muda mfupi baada ya Waingereza kuamua kujiondoa, viongozi wa Jumuiya hiyo wametangaza kukutana muda wowote kuanzia sasa kujadili uamuzi huo, kikao kinachokwenda kujadili mtikisiko huo ndani ya Jumuiya ya Ulaya.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!