WAKATI Watanzania wakijiuliza chanzo cha kukithiri kwa mauaji ya watu kuchinjwa, kumetokea tukio lingine, baada ya watu wanane wa familia tofauti, kuuawa kwa kuchinjwa usiku wa kuamkia jana kwenye kitongoji cha Kibatini, wilayani Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul, alisema watu wanaodhaniwa kuwa majambazi, walivamia kijiji hicho na kufanya mauaji hayo saa 7.00 usiku wa kuamkia jana. Watu waliouawa ni pamoja na Mjumbe wa Serikali ya Kijiji, Issa Hussein (50), Mkola Hussein (40), Hamisi Issa (20) na Mikidadi Hassan (70).
Wengine waliouawa kinyama ni raia wa Kenya aliyefahamika kwa jina moja la Mahmoud, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 na 40, Issa Ramadhani (25) na wachunga ng'ombe wawili waliofahamika kwa jina moja moja tu la Kadiri na Salum. Watu hao walikusanywa kutoka nyumba tofauti za kata ya Kibatini na kupelekwa sehemu moja ambako walichinjwa. Shuhuda wa miongoni mwa matukio hayo, Asha Said, ambaye ni mke wa marehemu, Mkola alisimulia kuwa watu hao walifika nyumbani kwao saa saba usiku wa kuamkia jana na kugonga mlango wa nyumba yao kwa nguvu huku wakiwaamuru watoke nje. “Watu hawa walivamia nyumbani na kutuamuru tutoke nje kwa kusema; `toka nje au tunavunja mlango’ baada ya kugonga sana na ndipo mume wangu alipoamua kutoka nje na wakamkamata na kumlaza chini huku wakimkanyaga kanyaga tumboni kisha wakamwambia waende naye kwa kaka yake Issa,” aliongeza Asha. Asha alisema wauaji hao walimchukua mume wake na kumpeleka kwa kaka yake ambaye ni Issa, ambaye pia aliuawa kwenye tukio hilo. Alisema walipofikishwa huko walianza kuwaulizia vijana saba, ambao walikuwa wamekamatwa na polisi kwenye eneo la Kibatini hivi karibuni. Vijana hao walikamatwa na polisi baada ya watu wa eneo la Kibatini kuwashuku mienendo yao na kuamua kuvitaarifu vyombo vya dola. Asha alieleza kuwa baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa Mkola na Issa waliwachinja mbele ya watu waliokuwa wanaishi karibu na Issa. “Waliwakusanya wote sehemu moja na kuamua kuwachinja pamoja lakini kubwa walikuwa wanataka kujua walikopelekwa vijana wao waliokamatwa,” aliongeza Asha. Naye shuhuda mwingine wa mauaji hayo, Kea Leonard (70), ambaye ni jirani yake marehemu Mkola alisema alisikia kishindo kikubwa mlangoni kwa jirani yake huku watu wakimtaka atoke nje na kuongeza walimhoji kuhusiana na vijana waliokamatwa na polisi hivi karibuni. "Wiki moja iliyopita kuna watoto saba umri kati ya miaka 10 na 13 walikuwa wakikimbia na ndipo walipofika huko bondeni wakakuta maji ya mto yamejaa wakashindwa kuvuka tulipowakamata walikuwa wanane lakini mmoja akakimbia baada ya kuwahoji na wao kushindwa kutoa maelezo yanayoeleweka ndipo tulipoamua kuwaita Polisi waliowachukua sasa ndiyo hao wanaowatafuta," alisema. MAELEZO YA POLISI Kamanda Paulo alisema majambazi hao walivamia nyumba ya Mkola na kisha baada ya kuua walikwenda nyumbani kwa Mikidadi Hassan na kumchinja kabla ya kummaliza Issa. “Watu hao walivamia nyumba hizo tatu na kuanza kuua kwa kutumia mapanga na visu,” alisema Kamanda Paulo. Kamanda Paulo aliongeza kuwa majambazi hao walipora bidhaa mbalimbali vikiwamo biskuti, sukari na mchele kwenye duka la Issa Hussein (marehemu ). Tukio hilo ni mfululizo wa matukio ya mauaji jijini Tanga ambapo Aprili 20, mwaka huu watu watano waliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi baada ya kuvamia duka la bidhaa za jumla la Central Bakery. Hivi karibuni uongozi wa Tanga ulitoa taarifa ya wahamiaji haramu waliojificha kwenye mapango ya Amboni mkoani humo. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, alikaririwa akieleza kuundwa kwa kikosi kazi cha Jeshi la Polisi kinachoshirikina na Jeshi la Wananchi (JWTZ ) kilichopewa kazi ya kufanya ya doria na kuwasaka watu hao ambao wamekuwa wakitoka mapangoni na kufanya uhalifu wakati wakitafuta chakula kwenye makazi ya wananchi. DIWANI AZUNGUMZA Diwani wa Kata ya Mzizima, Fredrick Chiluba, alisema hali hiyo imewatia hofu wananchi wa kata hiyo huku wakishindwa kujua hatma ya usalama wa maisha yao. “Hawa watu bwana wiki tatu zilizopita walivamia kijiji hicho na kuchinja kuku 40, mbuzi wawili na ng'ombe mmoja, sasa leo wamefanya haya kweli ni hali ya mashaka sana kwa wakazi wa eneo hili,” alisema Chiluba. Alisema hali hiyo imewafanya wananchi kuomba hifadhi kwenye maeneo ya shule ambayo wanadhani watakuwa salama zaidi kuliko majumbani mwao. “Wananchi wa Kibatini ambao ni 128 sawa na kaya 50 wameomba wapewe hifadhi kwenye shule kwa kuhofia usalama wao,” alisema. Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mleni, Shaban Mwamini alisema kuwa wakati umefika wa serikali kueleza bayana wahusika wa matukio hayo badala ya kuwaficha. “Hatuhitaji kuishi tena kwa matumaini watuambie waliopo huko mapangoni ni akina nani tuelewe kuliko kuambiwa ulinzi umeimarishwa wakati watu wanatufuata majumbani tutaishi hivi mpaka lini,” alisema Mwamini. MWENDELEZO WA MAUAJI YA KUCHINJA Tukio la Tanga ni la tatu kutokea nchini mwezi Mei, mwaka huu baada ya Mtumishi wa Wizara ya Fedha, Anetha Msuya (30) kuuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana katika eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, Mei 26, mwaka huu. Pia, Mei 19, mwaka huu watu 15 wakiwa wameficha nyuso zao walivamia msikiti katika mtaa wa Utemini wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza na kuwaua watu watatu kuwachinja kwa mapanga na mashoka baada ya kuwakuta wakiswali. Mkurugenzi wa Upelelezi anasemaje? Mkurugezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Diwani Athumani, alikaririwa na Nipashe juzi akisema uchunguzi wao umebaini kuwa chanzo cha mauaji mengi nchini ni kulipiza visasi, watu wanakuwa na tofauti za mali katika familia, mirathi, imani za kishirikina, uhalifu wa kawaida kugombania mali na ulevi. Alisema wanachosahau wanajamii kuwa zipo njia nyingi za kufuata kupata haki ikiwa ni pamoja na kwenda katika vyombo vya dola na baadaye mahakamani. “Tuko katikati ya operesheni, tunawasaka wote waliohusika na matukio ya hivi karibuni tunaamini watapatikana. Kabla hawajakamatwa ni vizuri wajisalimishe ili kukwepa kuisumbua serikali,” alisema. Aidha, aliiomba jamii inapoona watu wana nia ovu wanafanya mambo maovu kabla hayajatokea waseme, kwani leo wanaweza kufurahi kwa kuwa aliyepatwa ni mwingine, lakini kesho inaweza kuwa zamu yao.

No comments:
Post a Comment