Polisi katika mji wa Olarndo nchini Marekani, wanasema kuwa watu 50 waliuawa kweye shambulizi la risasi kwenye baa moja ya usiku.
Polisi wamethibitisha kuwa mshambuliaji huyo alikuwa na bunduki mbili, na aliwashika watu mateka na kufyatuliana risasi na polisi kabla ya kuuawa.
Maafisa katika jimbo la Florida wanasema kuwa wanalichunguza shambulizi hilo linalochukuliwa kuwa la kigaidi.
Zaidi ya watu 50 waliojeruhiwa wamepelekwa matibabu hospitalini
Baa ya Pulse ambapo shambulizi hilo lilitokea inajitambua kama ya wapenzi wa jinsia moja.
No comments:
Post a Comment