Watu watatu wanaodaiwa kuwachinja watu 8 katika eneo la Kibatini lililopo kata ya Mzizima jijini Tanga wameuawa na Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi katika majibizano ya risasi wakati walipokuwa wakitaka kutoroka baada ya kukamatwa kisha kuwapeleka askari katika pori kuwaonesha silaha aina mbali mbali walizokuwa wamezifukia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msadizi wa Jeshi hilo nchini Leonard Paul amesema silaha zilizokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na Jambia ambalo limetumika kuwachinja watu hao,SMG mbili, bastola moja yenye risasi 7 pamoja na risasi za SMG 35.
Baadhi ya wananchi wa Jiji la Tanga wakielezea hatua hiyo wamepongeza vyombo vya usalama kwa jitihada za kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu kutoka maeneo ya nje ya jiji la Tanga kwa kushirikiana na baadhi ya wakazi wa jiji
No comments:
Post a Comment