Sunday, 12 June 2016

WAJASILIMALI WATAKIWA KUTAFUTA SOKO KWA MTANDAO


Wajasiriamali wa tanga wakiwa katika maonyesho

WAJASIRIAMALI wanawake mkoani hapa wametakiwa kutafuta masoko kwa njia ya mitandao na kulitumia soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) ili kukuza biashara zao na kuwa wafanyabiashara wakubwa wa kimataifa.



Akizungumza katika kongamano la ufunguzi wa Tanga Women Gala, Tawi la Tanga hivi karibuni, Mratibu wa Gala, Lucy Mwinuka, alisema wajasiriamali wengi biashara zao zinashindwa kupata masoko baada ya kutegemea soko la mtu
mmoja mmoja.
Mwibuka alisema mfumo wa biashara mtandaoni unaweza kumuinua mjasiriamali na kuwa mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa hivyo kuwataka kubadilika katika karne hii ya utandawazi.
“Ndugu zangu lazima tubadilike na kuachana na dhana za kizamani na tuweze kuwa wajasiriamali wa kimataifa kama tutaitumia vema mitandao kutafuta masoko na kuzitangaza ndani na nje ya nchi kuweza kunufaika," alisema.
Aliwataka wajasiriamali hao pia kulitumia soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kujitangaza kama ambavyo wenzao wa Jumuiya hiyo wanavyotafuta masoko ili kufikia malengo makubwa.
Awali akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia ya Tree of Hope, Fourtunata Manyeresa, aliwataka wanawake kujishughulisha na kazi za mikono na kuacha kukaa majumbani na kuwategemea wanaume pekee.
Manyeresa alisema wanawake wanaweza fursa nyingi za kujikomboa na kuwa wajasiriamali wa kutegemewa hivyo ni wajibu wao wa kujiunga na vikundi na kuweza kupata mikopo.
Hata hiyo alisema kupitia shughuli za mikono zinaweza kuwakomboa kutoka katika limbi la umasikini lakini akiwataka kuweka utayari ikiwemo kuacha kuwategemea watu ambao hawawezi kuwakidhi shida zao kikamilifu.
“Ukiangalia hata mimi pia ni mjasiriamali na wakati mwingine mwenzangu akiwa hayupo naendesha maisha nyumbani na watoto wanaenda shule bila shida yoyote, nanyi nawaomba tujifunge vibwebwe kwa pamoja na kupeana
mbinu za kujikomboa,” alisema.

Alisema ili wanawake wajikomboe kutoka katika umasikini ni lazima wawe tayari kujishughulisha na kazi ambazo watajipatia kipato halali na kutafuta masoko.
NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!