Monday, 13 June 2016

Unataka kuoa raia wa kigeni? Soma hii



Ngara. Watanzania wanaotaka kuoa raia wa kigeni wanapaswa kulipa Sh1.3 milioni kama gharama za kibali cha kuishi na mwenza hapa nchini.



Kaimu Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Ngara, Fadhili Zeyumba amesema kibali hicho kinatakiwa kulipiwa kwa miaka miwili, vinginevyo anayebainika kuishi na mhamiaji anatozwa faini au kifungo cha miaka miwili gerezani.
Onyo hilo la Zeyumba linakwenda sambamba na lile lililotolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Honoratha Chitanda aliyewataka raia wa kigeni wanaoishi kinyume na utaratibu kuondoka, la sivyo watakamatwa na kufikishwa mahakamani.
“Acheni kuwakaribisha wahamiaji haramu kumbuka kikulacho kinguoni mwako baadhi yao wanahatarisha usalama wa wilaya yetu na kusababisha matukio ya uhalifu wafuate taratibu za kuingia nchini,”alisema Chitanda.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!