Thursday, 2 June 2016

UN YAISHUKURU TANZANIA KWA JUHUDI ZAKE ZA KUSAIDIA KULINDA AMANI NCHI ZINGINE‏

 Mgeni rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akipata maelezo mara baada ya kuwasili kwenye  maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)


 Kutoka kushoto ni Mgeni rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa, Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirikala Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama pamoja na Mkuu wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali, Elias Athanas wakitoa heshima kwa wimbo wa taifa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
 Mgeni rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
 Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akisoma hotuba pamoja na ujumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
 Mgeni rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akiweka shada la maua kwenye mnara wa mashujaa kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini kulinda amani ya mataifa mengine yenye machafuko wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
 Mkuu wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali, Elias Athanas akiweka shada la maua kwenye mnara wa mashujaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
 Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akiweka shada la maua kwenye mnara wa mashujaa kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha katika oparesheni ya kulinda amani katika nchi zenye machafuko wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
 Mkuu wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali, Elias Athanas akisalimiana na Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirikala Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama mara baada ya kuwasili katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016. Katikati ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Brass Band ikiongoza gwaride maalum la askari walinda Amani kuingia viwanja wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.



 Baadhi ya viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Balozi wa nchi mbalimbali pamoja na viongozi wa Dini waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.

Na Mwandishi wetu
Katika kutambua kujitolea kwa Tanzania kutoa askari wake kwenda kulinda amani katika nchi zingine, Umoja wa Mataifa (UN) umesema unatambua huduma inayotolewa na Tanzania ikiwa kama mwanachama wa UN na unafurahishwa na hatua iliyopo ya kuendelea kusaidia kulinda amani katika operesheni zinazofuatia.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ambapo kwa nchini siku hiyo iliadhimishwa Dar es Salaam katika Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja
Manyama alisema Tanzania imekuwa ikijitolea kusaidia ulinzi wa amani katika mataifa mengine licha ya kupoteza baadhi ya wanajeshi wake lakini bado wamekuwa wakiendelea kujitolea kusaidia kuimarisha ulinzi wa mataifa mengine ambayo hali ya usalama inakuwa siyo ya uhakika.

“Tumefurahishwa na historia ya Tanzania ya kuzisaidia nchi jirani kulinda amani na kutatua migogoro ya hapo zamani na kuziwezesha kujipatia uhuru,” alisema Manyama.

Aidha Manyama alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukijitahidi kuendelea kushirikiana na wanachama wake ili kwezesha upatikanaji wa amani kwa mataifa yote na itaendelea kutoa heshima yake kwa wanawake na wanaume ambao walipoteza maisha wakiwa kazini kulinda amani ya mataifa mengine.

“Mwaka jana idadi ya waliokufa ilikuwa 129, walinda amani hawa walitoka katika nchi 50, wakiwa ni pamoja na wanajeshi, polisi, watumishi kutoka mataifa mbalimbali, wafanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa na watumishi wa ndani,

“Tunapenda kutoa heshima kwa mashujaa wetu zaidi wanaume na wanawake milioni moja waliotumikia chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa kwa majivuno, weledi tangu kuanza kwa kazi hiyo 1948,” alisema Manyama.

Nae mgeni rasmi katika siku hiyo, Meja Jenerali James Mwakibolwa aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa jinsi wanavyofanya kazi na kusaidia kuokoa maisha ya watu wengi na kuahidi Tanzania itaendelea kutoa wanajeshi wake ili waendelee kulinda amani.

“Tumeshatoa walinda amani 2,328 katika operesheni mbalimbali zilizopita na tutandelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha amani na utulivu katika maeneo mengine,” alisema Meja Jenerali Mwakibolwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!