Kwa kweli wanawake tunanyanyaswa sana, sasa hapa hakuna hata wakumzuia huyu baba anayefanya unyama huu? wanaume wanatakiwa waanze kuelimishwa upyaa, elimu ndogo ndio tatizo! yaani anaona ufahari kumpiga mwanamke hivi, na watu wamemzunguka, siajabu kuna wanaoshangilia hapo kwamba huyo mama apigwe tu! hivi lini wanawake wa Afrika watakuwa na thamani na kuwa huru? mara wanabakwa, kupigwa vipigo visivyo na kikomo, wanachinjwa hovyo, Hivi serikali inayaona haya?Serikali inachukuliaje unyama kama huu? yaani jitu kama hili libaba wako wengi tu hasa vijijjini.
Wanawake wa vijijini wanakumbana na unyama kama huu kila kukicha, na unakuta muhusika yupo tu anaendelea kuishi kwa raha mustarehe! mijitu kama hii ni ya kunyongwa tu!
Umoja wa wanawake na taasisi mbalimbali zinazohusika, wakumbukeni wanawake kama hawa, na haswa vijijini. unyama kama huu hauvumiliki!

No comments:
Post a Comment