Thursday, 23 June 2016

SALAD ITAKAYOKUSAIDIA KUKATA MAFUTA MWILINI .



Maparachichi ni matunda muhimu sana kama unajaribu kupunguza uzito. 
Japokuwa yana mafuta, mafuta yake humeng'enywa kirahisi tumboni na hayapelekei kuongezeka uzito. Yanashibisha kwa muda mrefu na hivyo kukuzuia kula kupita kiasi.



 Pia yana virutubisho vinavyopelekea kuchomwa mafuta mwilini zaidi. Kwa kifupi, parachichi ni moja kati ya matuda bora kabisa duniani ya kula mara kwa mara ili kupungua uzito kisha kumaintain. Na kupitia salad hii unaweza kutumia fursa kuongeza mbogamboga na matunda mengine yanayosaidia katika kupunguza uzito kama matango na mbogamboga zozote za majani (mbichi au zilizochemshwa).
Uandaaji:
- Vipande 4 vya vitunguu vilivyokatwa kwa mviringo
- Machungwa 2
- Maparachichi 2
- Vijiko 3 vya chai vya mafuta ya zeituni (olive oil)
- Vijiko 2 vya chai vya majani ya mint
- Kijiko 1 cha chai cha maji fresh ya ndimu
- Kijiko robo cha chai cha chumvi
Loweka vitunguu, ukali utoke. Menya machungwa na ondoa kabisa ule weupe ibaki nyama tu. Katakata kwa vipande vya mviringo. Menya na katakata maparachichi upendavyo. Ongeza majani ya mint. Ongeza mafuta ya olive ukipenda kwa ajili ya kuongeza ladha. Mwagia maji ya ndimu. Enjoy.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!