Tuesday, 28 June 2016

POLISI KUWATAJA WALIOMCHINJA DADA WA BILIOEA MSUYA



Polisi kuwataja watuhumiwa waliomchinja dada wa Msuya
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema litaanika wahusika walioshiriki katika mauaji ya Anethe Msuya, ambaye ni dada wa aliyekuwa mfanyabiashara bilionea mkoani Arusha, Erasto Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi.





Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishna Saimon Sirro, alisema uchunguzi wa mauaji hayo umefikia hatua nzuri na muda si mrefu wahusika watatajwa hadharani.

“Naomba nizungumzie suala la Anethe Msuya, mpaka sasa tumefikia pazuri na siku si nyingi wahusika tutawaweka hadharani japokuwa kwa sasa siwezi kuwataja,” alisema Kamanda Sirro.
Anethe aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana Mei 26, mwaka huu, nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, huku wauaji hao wakifanya hivyo pasipo kuchukua chochote na kutoweka.
Mauaji ya Aneth ni mwendelezo wa mauaji yanayoikumba familia hiyo ya Msuya baada ya kaka yake mfanyabiashara maarufu wa madini kuuawa Agosti 7, 2013 kwa kupigwa risasi katika eneo la Mijohoroni, wilayani Hai, mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!