Msichana Mary Kibwana Kamango (pichani) raia wa Kenya ambaye alinyanyaswa na kujeruhiwa na mwajiri wake huko nchini Jordan amerejeshwa nyumbani.
Mary amesimulia kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa wasichana kutoka Afrika wanaofanya kazi za ndani katika nchi zilizopo katika Falme za Kiarabu.
Tukio lake lilihusisha kupigwa na mwajiri wake na kuchomwa kwa moto wa gesi mapema mwezi Aprili mwaka huu. Pamoja na kuomba msaada hakuna aliyemsaidia ikiwemo vyombo vya usalama nchini Jordan.
Baada ya tukio hilo la kusikitisha, raia wa Kenya wanaoishi katika nchini Jordan walichangishana fedha za nauli na kufanikiwa kumsafirisha mwenzao kurudi nyumbani. Kwa sasa Mary amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta ambako anapatiwa matibabu ya majeraha ya moto wa gesi.
Mary amewaasa wasichana wenzie dhidi ya unyanyasaji wanaofanyiwa wafanyakazi wa kazi za ndani katika nchi za Falme za Kiarabu.
DAR24.
No comments:
Post a Comment