Tuesday 14 June 2016

Mkesha wa kuwaenzi waathiriwa wa Orlando wafanyika

Image copyright
Image captionMkesha Orlando
Mkesha umefanyika huko Orlando mjini Florida pamoja na maeneo tofauti duniani ili kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio katika kilabu moja ya usiku ya wapenzi wa jinsia moja.


Kiongozi mmoja wa kiislamu aliwaambia wale wanaohudhuria mkesha huo kwamba Waislamu wanaungana nao kupinga chuki ,mauaji na uharibifu.
Mikutano kama hiyo pia ilifanyika katika mataifa kama vile Ufaransa,Australia Uingereza na Ujerumani.
Shambulio hilo la kilabu ya usiku lilisababisha mauaji ya watu 49 huku makumi wakijeruhiwa .
Image copyright
Image captionOrlando
Mamlaka nchini Marekani inasema kuwa mshambuliaji Omar Mateen aliahidi utiifu kwa kundi la wapiganaji wa Islamic State muda mfupi kabla ya shambulio hilo.
Wateja kadhaa wa Pulse wameviambia vyombo vya habari nchini Marekani kwamba Mateen alikuwa akiingia katika kilabu hiyo mara kwa mara.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!