Misri imesema kuwa itachunguza madai kwamba mmoja wa maafisa wake aliwaita Waafrika wanaoishi katika jangwa la sahara kuwa ''mbwa na watumwa'' wakati wa mkutano jijini Nairobi.
Madai hayo yametajwa na mwana
diplomasia wa Kenya ambaye anasema Misri inafaa kuzuiliwa kuwakilisha Afrika katika majadiliano yoyote.
Lakini Cairo imesema kuwa hakuna ishara kwamba lugha kama hiyo ilitumika na kutaka ushahidi wowote uliorekodiwa kutolewa.
Kisa hicho huenda kikazua wasiwasi kati ya Msri na majirani zake wa Jangwa la Sahara.
Katika malalamishi rasmi,Yvonne Khamati ,mwenyekiti wa kamati ya kiufundi ya wanadiplomasia wa Afrika amesema kuwa kuwa matamshi hayo yalitolewa na kiongozi wa ujumbe wa Misri katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wiki iliopita.
''Kulikuwa na mgawanyiko katika mkutano huo baada ya makubaliano ya Gaza kutoidhinishwa kutokana na ukosefu wa wanachama'',alisema Khamati.
''Matamshi hayo yaliotolewa kwa lugha ya Kiarabu yalitolewa katika mazungmzo na ujumbe wa Misri'',aliongezea Bi Khamati.
BBC.
No comments:
Post a Comment