Tuesday 14 June 2016

MIKATE MIDOGO (EASY BUNS)



VIPIMO:
Unga wa ngano vikombe 3 1/4
Sukari vjk 2 chakula
Chumvi kjk 1 chai
Hamira vjk 3 chai
Maziwa ya unga vjk 2 chakula (ukipenda)
Maji vugu vugu kikombe 1 1/4
Siagi vjk 2 chakula




NAMNA YA KUPIKA
1. Tia mahitaji yote katika bakuli isipokuwa siagi kisha kanda kwa dk 5.

2. Tia siagi kisha kanda unga wako kwa dk 10 hadi uwe mlaini na wakuvutika.

3. Tia katika bakuli ulopaka mafuta au siagi, funikia na plastic au kitambaa acha ufure kwa muda wa dk 30.

4. Kanda kwa dk 1 kisha gawa vipande na kisha fanya maduara. Panga katika tray ulopaka mafuta.

5. Funikia tena acha zifure kwa dk 30. Oka katika oven ya moto joto 180°c kwa muda wa dk 20 au hadi zipate rangi ya brown juu.

6. Paka siagi juu zikiwa bado moto. Enjoy!

Note:
Weza paka egg wash juu ya buns kabla ya kuoka (piga yai 1+ kjk 1 Maji)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!