Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo wakati alipokuwa anawasili msibani katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga, ambapo watu wanane walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi.
Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia hizo zilizofiwa katika kitongoji hicho. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwapa pole wanafamilia ya marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane zilizofiwa katika kitongoji hicho. Nyuma ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo akiwaonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wapili kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (watatu kushoto), nyumba ya kwanza katika Kitongoji cha Kibatini walioivamia watu wanaohofiwa kuwa majambazi na kufanya mauaji. Naibu Waziri na Viongozi hao walienda kutoa pole katika familia zilizofiwa katika Kitongoji hicho kilichopo katika Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa salamu za pole kwa ndugu wa marehemu Mkola Hussein pamoja na wananchi wa Kitongoji cha Kibatini kulipotokea mauaji kwa watu wanane ambao walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji hicho kilichopo Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Katika hotuba yake Masauni alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo na itahakikisha inawakamata wauaji wote waliofanya ukatili huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange kabla ya kwenda kutoa pole kwa familia ya wafiwa katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga ambapo watu wanane walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment