Dar es Salaam. Uamuzi wa Mahakama ya Kisutu baadaye Mahakama Kuu, uliomuondolea aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya na wenzake shtaka la kutakatisha fedha, umefutiliwa mbali na Mahakama ya Rufani.
Kutokana na hatua hiyo, Harry Kitilya na wenzake, Shose Sinare na Sioi Solomonali, wataendelea kusoma rumande.
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alikata rufaa kupinga uamuzi wa kuwaondolea shtaka hilo, hivyo, Mahakama ya Rufani iliamuru rufaa ya DPP kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu isikilizwe upya na Mahakama Kuu mbele ya jaji mwingine, tofauti na Jaji Moses Mzuna aliyeitupilia mbali.
Mbali na shtaka hilo, Kitilya na wenzake wanakabiliwa na mashtaka mengine saba ya kughushi, kutoa nyaraka za uongo na kujipatia dola 6 milioni za Marekani
MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment