Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro ametoa wito kwa wamiliki wote wa nyumba jijini Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanaweka kipengele cha kuwepo na picha katika mikataba ya kupangisha nyumba zao kutokana na uwepo wa wimbi la uhalifu jijini.
Aidha amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na wao kuwa na picha za wapangaji wa nyumba hizo kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuweza kuwabaini wahalifu katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment