Thursday, 23 June 2016

Irene Uwoya Kusomesha Watoto 10


NYOTA wa filamu za Tanzania, Irene Uwoya, amechangia katika mfuko wa binti ili kusaidia kusomesha watoto 10 kati ya wengi wanaoishi kwenye mazingira magumu.




Uwoya alitoa mchango huo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuhitimisha matembezi ya kuchangisha fedha na vifaa vya shule kwa watoto wanaoishi mazingira magumu.
“Nimejitolea kusomesha watoto hao 10 kupitia ‘Binti Foundation’ ili nifanikishe ndoto zao kwani ukimsomesha msichana ni sawa na kusomesha jamii nzima hivyo nitagawana nilichonacho katika kuhakikisha nafanikisha hilo,” alisema Uwoya.
Aidha, Uwoya alisema licha ya kusomesha watoto hao atatumia kipaji chake cha uigizaji kutoa elimu juu ya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kumpatia elimu mtoto wa kike na madhara ya ukatili wa kijinsia.
Mtanzania

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!