Uamuzi huo unakuja wiki moja baada ya hospitali hiyo kutoa taarifa za utaratibu huo mpya wa huduma ya chakula kwa wagonjwa ambapo kila mgonjwa alitakiwa kutoa Sh 6,000 kwa mlo wa siku.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam.
Alisema amechukua uamuzi huo baada ya kupokea maoni kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali.
“Nimechukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa utaratibu huo umeleta wasiwasi kutokana na maoni tuliyopokea kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wa afya,” alisema Mwalimu.
Aidha, Mwalimu alisema kuwa taarifa hiyo imesababisha kuwepo kwa mkanganyiko juu ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa watu wanaohudumiwa na bima ya afya jambo ambalo linatakiwa kutolewa ufafanuzi.
“Utaratibu huo utasubiri kwa muda wa mwezi mmoja ili mambo yapangwe na kutolewa ufafanuzi zaidi hasa kwa watu wanaotumia bima za afya ambao pia wanatakiwa kuchangia ili kuwezesha kuboresha utoaji wa huduma hiyo,” aliongeza Mwalimu.
Pia Waziri huyo alisema kwenye fedha hizo kila mgonjwa atatakiwa kutoa Sh. 50, 000 ambayo itagawanywa katika sehemu tatu.
“Mgonjwa akitoa elfu 50,000¸ 10,000 itakuwa kwa ajili ya kumuona daktari, 10,000 kwa ajili ya dawa na 30,000 ambayo itaingia katika huduma ya chakula kwa kipindi ambacho mgonjwa atakuwa hospitalini,” alisema Mwalimu.

No comments:
Post a Comment