Imeelezwa kwamba , upatikanaji wa vifaa saidizi ( assistive divices) kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali siyo tu, utawawezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi, kijamii na maendeleo bali pia utawaondolea hisia za kunyanyapaliwa na kubaguliwa.
Hayo yameelezwa na siku ya jumatano na Dkt. Abdallah Possi ( Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri, wakati alipokuwa akichangia majadiliano kuhusu mada ya uondoaji wa umaskini na kukosekana kwa usawa kwa watu wote wenye ulemavu. Mhe Possi alikuwa mmoja wa wanajopo watano, walioongoza majadiliano kuhusu mada hiyo katika siku ya pili ya mkutano wa tisa wa Mkataba wa Watu Wenye Ulemavu unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Katika mchango wake, Naibu Waziri amesisitiza kwamba suala la upatikanajji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ni muhimu sana kwa kile alichosema ukosefu wa vifaa hivyo ni moja wa changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu.
Akatoa wito kwa serikali, jumuiya ya kimataifa na asasi za kiraia kuangalia ni kwa namna gani katika wa umoja wao wanaweza kushirikiana ili kukabili changamoto hiyo ya upatikanaji wa vifaa saidizi wa watu wenye ulamavu.
Mhe Possi anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu, pamoja na kuzungumza uhaba wa vifaa saidizi pia amezungumzia kwa uzito wa aina yake kuhusu pamoja na mambo megine fursa ya upatikanaji wa ajira kwa watu wenye ulemavu, unyanyapaji na mitizamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu.
Akasema mitizamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu, ubaguzi na uyanyapaji umekuwa kikwazo kikubwa katika siyo tu, utekelezaji wa sera na mipango ikiwamo ya fursa za ajira kwa walemavu, bali pia katika kufungua fikra na mitizamo mipana na jumuishi kuhusu watu wenye ulemavu.
Aidha Mhe. Naibu Waziri amerejea kauli yake kwamba inakuwa vigumu kutenganisha ulemavu na umaskini kwa kile anachosema vinakwenda pamoja.
Akasisitiza ili watu wenye ulemavu waweze kushiriki katika utekelezaji wa Agenda 2030, kujipatia fursa za ajira kama ilivyo kwa watu wengine pamoja na kuondokana na umaskini, jamii inao wajibu mkubwa wa kutoa ushirikiano kuacha kuwabagua, kutowanyanyapa na kubwa zaidi kwa watendaji na wenye mamlaka serikali kuandaa na kutekeleza mipango ambayo ni jumuishi na yenye kuzigatia maslahi , mahitaji na mazingira halisi ya watu wenye ulemavu.
Hoja ya vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu iliungwa mkono na wanajopo wengine kwa kile walichoeleza kwamba ni muhimu sana katika kuwafanya watu wenye ulemavu kuwa huru na kuondokana na utegemezi.
Wanajopo hao mbali ya Dkt. Possi walikuwa ni Bi. Asa Regner, Waziri wa Waziri wa Watoto, Wazee na Usawa wa Jinsia kutoka Sweden, Bw. Joelson Dias ambaye ni Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati ya Haki za watu wenye ulemavu kuotka Brazil, Bi, Silvia Quam kutoka Guatemala na Bi Emi Aizawa, kutoka Japan.
KWA HISANI YA THE NKOROMO BLOG.
No comments:
Post a Comment