WIZARA wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inatarajia kuwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote mwezi Septemba mwaka huu, unaolenga kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na bima hiyo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, wakati akizundua Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Bodi hiyo inaongozwa na Spika Mstaafu, Anne Makinda.
Alisema lengo la Muswada huo pia ni kufikisha huduma kwa asilimia 50 au zaidi kwa Watanzania wote ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 28 ya wananchi wanaotumia huduma kwa sasa.
“Mimi nataka mjiandae na kuweka mikakati madhubuti kwa falsafa ya hapa kazi tu. Tunataka kuwahudumia Watanzania wengi zaidi kupitia Bima ya Afya, kabla na baada ya kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Bima kwa wote,” alisema.
Alisema hataki kuona kutokuwa na fedha au uwezo wa kuchangia huduma za matibabu kunakuwa kikwazo cha wananchi kutopata huduma muhimu hasa dawa.
Aidha, alisema serikali inatambua kuwa upatikanaji wa huduma bora za matibabu hasa kwa wananchi wa kawaida ni pamoja na upatikanaji wa huduma ya dawa ambazo takribani asilimia 80 tunaziagiza kutoka nje ya nchi.
Alibainisha kuwa, wananchi wanaridhika wanapopata huduma ya matibabu na kupatiwa dawa hivyo pia wameweka mikakati ya kuhakikisha zinapatikana kwa wingi nchini.
Sambamba na hilo, Mwalimu aliagiza asilimia 25 ya fedha za marejesho ya madai ya watoa huduma wa mfuko wa bima ya afya kwa hospitali zilizo katika kanda 52 zipelekwe moja kwa moja katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
“Najua Hospitali hazitakubali suala hili licha ya kuwa nilishaagiza, naagiza tena NHIF hakuna kupeleka asilimia 100 ya fedha za matibabu mnazodaiwa na hospitali na badala yake pelekeni asilimia 75 na asilimia 25 pelekeni MSD ili watoe dawa hospitalini,” alisema Mwalimu.
Pia alisema katika bajeti ya serikali ya mwaka huu, wamepata Sh. Bilioni 251 fedha ambazo hazijawahi kutolewa kwa wizara hiyo na kwamba zitawezesha utoaji huduma kwa akina mama na kuongeza dawa hospitalini.
Mwalimu alisema pia wameagiza MSD kukamilisha utaratibu wa kununua dawa kutoka kwa watengenezaji badala ya kununua kwa wasambazaji wakubwa.
“Wakati Wizara ikichukua hatua hizi, niombe bodi yako iangalie namna bora ambayo mfuko utashiriki kuwekeza katika eneo la viwanda na dawa,” alisema.
Alisema mfuko ukishiriki kuwekeza katika viwanda vya dawa hasa za msingi kutasaidia upatikanaji wa huduma, kupunguza malalamiko kwa wanachama wake, kuongeza ajira na kupunguza matumizi ya fedha chache za kigeni kwa ajili ya kununua dawa hizo nje ya nchini.
Mwalimu pia aiitaka bodi hiyo kuchunguza malalamiko ya wananchi juu ya utoaji huduma uliotofautiana kati ya watumiaji wa kadi za NHIF na wale wa Jubilee ambao wamekuwa wakipata huduma nzuri kuliko wenzao.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Benard Konga, alisema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo pamoja na kuendeleza juhudi za kuwa na wanachama asilimia 50 ifikapo mwaka 2020.
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Anne Makinda, alisema kama kiongozi wa bodi hiyo wataangalia namna ya kupata ufumbuzi wa tatizo la dawa.
Alisema pia bodi itafuatilia kipaumbele hicho pamoja na miongozo ya sera za uhai wa mfuko huo ili watu wengine wajiunge kwa kutoa elimu ya kutosha na kuboresha miundombinu.

No comments:
Post a Comment