WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mwaka wa fedha 2016/17 imepanga kukusanya Sh.bilioni 111.77 kutokana na shughuli za sekta ya ardhi na imepanga kutumia Sh. bilioni 20 kwa matumizi ya maendeleo.
Wizara hiyo imeliomba Bunge kuidhinisha Sh. bilioni 61.9 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/17.
Waziri Lukuvi alisema kati ya Sh. bilioni 61.9 wanazoomba, matumizi ya kawaida ambayo ni kulipa mishahara ni Sh. bilioni 16.3, na Sh.bilioni 25.5 kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Alisema katika fedha za matumizi ya maendeleo, Sh.bilioni10 ni fedha za ndani, na Sh. bilioni 10 ni fedha za nje.
“Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara iliidhinishiwa Sh. bilioni 72, kati ya fedha hizo Sh. bilioni 14.26 ilikuwa kwa ajili ya mishahara, Sh. bilioni54.64 kwa ajili ya matumizi mengineyo, Sh.bilioni3.46 miradi ya maendeleo, lakini Wizara ilipewa Sh.bilioni 42.81 tu,” alisema Lukuvi.
Kadhalika, Lukuvi alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 wanatarajia kukusanya Sh.bilioni 111.77 kutokana na kodi, tozo na ada mbalimbali zinazotokana na shughuli za sekta ya ardhi.
Lukuvi alisema endapo Sh.bilioni 111.77 zitakusanywa zitatumika kupanga na kupima viwanja na mashamba takribani 400,000 na kuwapatia wananchi hati miliki.
Alisema pia zitatumika kuhimiza wamiliki wote wa ardhi kulipa kodi ya ardhi kwa mujibu wa Sheria, pia kukamilisha na kutoza kodi ya ardhi kwa wenye leseni za vitalu vya kuchimba madini kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini.
Matumizi mengine ni kuhuisha viwango vya kodi ya ardhi kwa mashamba ya biashara yaliyoko nje ya miji yaliyomilikishwa chini ya Sheria namba nne ya mwaka 1999.
Lukuvi alisema kwa mwaka 2016/17 serikali imetenga Sh.bilioni tano kwa ajili ya kuanzisha Mfuko wa Fidia na kugharamia shughuli za Bodi ya Mfuko wa Fidia.
Alisema serikali pia inakusudia kusajili hatimiliki na nyaraka za kisheria 450,500 kati ya hizo hati za kumiliki ardhi ni 400,000, hati za kumiliki sehemu ya jengo 2,500 na nyaraka za kisheria 48,000.

No comments:
Post a Comment