Tuesday, 17 May 2016

Wanaotelekeza watoto kushughulikiwa



watoto wa mitaani ambao wametelekezwa na wazazi.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala, amesema serikali ina mipango mbalimbali ya kuwabaini wanaume wanaotelekeza familia na vitendo vingine vya unyanyasaji.





Akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM), Prosper Mbena, alitaka kujua mpango wa serikali wa kuwabaini wanaume hao na kuwafikisha mahakamni kwa kosa la kuwatelekeza watoto na kuwasababishia mateso, Dk. Kigwangala alisema serikali imejiwekea mikakati kadhaa ya kukabiliana na tatizo hilo.
Aliitaja mipango hiyo kuwa ni pamoja na mpango wa mwitikio wa kitaifa wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto wa mwaka 2013-2016 na mpango wa kuzuia ukatili dhidi ya wanawake wa mwaka 2005-2015.
“Mipango hiyo inaunganishwa kuwa mpango mmoja wa kitaifa ili kukidhi haja za upatikanaji wa taarifa zinazihusu ukatili dhidi ya watoto na wanawake, ikiwamo utelekezaji wa familia,” alisema.
Alisema kupitia mpango huo, serikali itahamasisha jamii kuibua vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo.
Aidha alisema Wizara imeanzisha mtandao maalum wa mawasiliano kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali za ukatili dhidi ya watoto.

NIPASHE.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!