Wednesday, 18 May 2016

VITUMBUA




Mahitaji:-
Mchele wa (vip) vikombe 2 
Hamira kjk 1 chai
Tui la nazi kikombe 1
Ute wa mayai 2 (ukipenda)
Sukari kikombe 1
Unga wa ngano kjk 1 chakula
Hiriki kjk 1 chai 




MATAYARISHO NA JINSI YA KUPIKA.
1. Loweka mchele katika maji usiku mzima.

2. Chuja maji yote kisha utie mchele katika blender pamoja na tui la nazi,unga wa ngano,hiriki na hamira.

3. Saga hadi uwe laini. Mimina katika bakuli,funikia acha sehemu yenye joto ufure hadi ujae mara mbili.

4. Tia sukari na ute wa yai koroga vizuri kuchangananya. Choma vitumbua vyako ktk moto wa kiasi hadi vipate rangi ya brown pande zote 2. Enjoy!

Note:-
Kama uji ni mzito sana ongeza maziwa au tui la nazi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!