Arusha. Polisi mkoani Arusha inawashikilia watu tisa kwa kosa la kuuza sukari tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema leo kuwa watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na watashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.
Mkumbo alisema mmoja wa watu hao amekutwa akiuza kwa Sh5,000 kwa kilo moja.
Alisema wengine walikamatwa wakiuza sukari Sh6,200; Sh3,000; Sh2,500 na Sh4,500 kwa kilo.
Kamanda Mkumbo amesema kamatakamata ya watu wa aina hiyo ni endelevu na aliwashauri wafanyabiashara wote mkoani Arusha kuuza sukari kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.
No comments:
Post a Comment