Tuesday, 10 May 2016

SUMATRA yatangaza nauli mabasi yaendayo kasi


Dar es Salaam. Hatimaye Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) yatangaza nauli zitakazo tumika kwa mabasi yaendayo kasi kuwa ni 400, 650 na 800 kwa safari za Mbezi mwisho hadi Kivukoni.


Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Giliard Ngewe amesema nauli kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya Kimara kwenda Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo - Kivukoni.
Amesema nauli ya Sh800 Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.
“Chombo chochote cha usafiri hakitaruhusiwa kutumia barabara za mwendo kasi kuanzia kesho, watakao kiuka agizo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa reseni za biashara zao” amesema.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!