Sunday, 1 May 2016
SHERIA 15 ZA MPIRA ZA KIPINDI CHA UTOTONI.
1. Mkubwa Hachezi Na Akicheza
Mnaingia Wawili.
2.Mwenye Mpira Hatolewi Hata
Akicheza Vibaya.
3.Inaruhusiwa Kubadili Kipa Kama
Penati Imetokea Na Baada Ya Penati
Anaruhusiwa Kurudi Wa Mwanzo.
4.Yule Mtaalam Wa Soka Hakosi
Namba Hata Siku Moja.
5. Dogo Mnene Lazima Awe Golikipa.
6.Mwenye Mpira Ataamua Nani
Asicheze.
7.Penati Itatokea Tu Pale Mchezaji
Akiumia Sana Na Kutoka Damu
.
8.Mechi Itaisha Kama Kila Mchezaji
Atakuwa Amechoka.
9. Hakuna Free Kick,refa Wala
Offside.
10. Ukichaguliwa Mwishoni Ujue
Uwezo Wako Mdogo Kuliko Wote
Uwanjani.
11.Mtaalam Wa Timu Akipewa Kazi
Na Wazazi Wake Lazima Mumsaidie
Ndo Mwende Kucheza.
12.Ukiumia Kidonda Kinawekwa
Mchanga.
13.Kipa Anaruhusiwa Kudaka Popote.
14. Wale Ambao Wamekosa Namba
Kazi Yao Ni Kufata Mipira Ikitoka.
15. Mwenye Mpira Akikasirika Mechi
Ndo Inakuwa Imeisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment