Taarifa iliyonifikia kutokea Mwanza ni hii ya kusikitisha ya watu watatu kuuawa kwa kuchinjwa wakiwa katika nyumba ya ibada usiku May 18, 2016, Msikiti wa RAHMANeneo la Ibanda relini mtaa wa Utemini Mkolani Mwanza.
Ripoti kutoka kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza Ahmad Msangi amesema……>>>Watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia mavazi ya kuficha uso, wakiwa na Mapanga, Shoka na Bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia msikitini wakati waumini wakiwa wanaswali wakazima taa wakisema Kwanini mnaswali wakati wenzenu wanashikiliwa na Polisi?’
‘Waliouawa 1.Feruz Ismail Elias (27) Imamu wa Msikiti, 2.Mbwana Rajabu (40), 3.Khamis Mponda (28) pamoja na Ismail Abeid (13) aliyejeruhiwa mwanafunzi wa shule ya Jabar Hila Nyasaka, anapata matibabu kwenye Hospital ya Nyamagana;- Kamanda Ahmad Msangi
‘Waumini wengine walifanikiwa kukimbia huku wahalifu wakikimbia na kurusha chupa mbili za Konyagi ndani ya Msikiti zikiwa na Petroli pamoja na tambi moto, chupa moja ililipuka ila haikuleta madhara makubwa’; – Kamanda Ahmed Msangi
No comments:
Post a Comment