RAIS John Magufuli leo anatarajiwa kutangaza kupunguza kodi ya PAYE kwa wafanyakazi, hatua ambayo moja kwa moja itaongeza mishahara kama, ikiwa moja ya hatua ya kuwaletea unafuu wa maisha.
Leo Rais Magufuli atakutana uso kwa uso na wafanyakazi kwenye sherehe za Mei Mosi kitaifa mjini Dodoma, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria sherehe hizo tangu aingie Ikulu Novemba 5, mwaka jana.

Upunguzaji wa kodi ya PAYE ni ahadi kubwa ambayo Rais Magufuli alikuwa akiitoa alipokuwa kwenye mikutano yake ya kampeni kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
Mara kadhaa Rais Magufuli alikuwa akiahidi neema kwa wafanyakazi kwa kusema atawalipa mishahara inayoendana na hali halisi ya maisha, akisema kuwa kiasi wanacholipwa sasa hakiwatoshi.
Kwenye mikutano yake hiyo ya kampeni, mara kadhaa Rais Magufuli alinukuliwa akielezea kusikitishwa na namna mishahara ya wafanyakazi ilivyo midogo na kwamba makato ya kodi nayo huwafanya waumie zaidi.
Aidha, akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wilayani Chato, Mkoani Geita Machi 26, Rais Magufuli alisema serikali yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo.
MKAO WA KULA
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Gratian Mukoba, alisema wafanyakazi wamekaa mkao wa kula kusubiri tangazo la Rais Magufuli kushusha kodi na kupandisha mishahara kama ambavyo amekuwa akiahidi.
Alisema Shirikisho hilo linapendekeza mshahara wa kima cha chini upande kutoka Sh. 300,000 hadi Sh. 750,000 ili wafanyakazi waweze kuishi maisha ya staha kama wengine.
Alisema kwa kuwa Rais Magufuli amefuta fedha za maadhimisho, semina, chai, safari na makongamano, anaamini serikali ina fedha za kuwafuta machozi wafanyakazi kwa kupunguza mzigo uliowaelemea.
Alisema kwa kuwa Rais Magufuli bado anakusanya nguvu na kuijenga upya serikali yake anaweza asifikie kiwango ambacho wao wamependekeza, lakini wanamshauri akishindwa kabisa angalau aongeze mshahara hadi Sh. 500,000.
“Kuna tofauti kubwa sana ya mshahara, wengine wanapata mishahara minono ya hadi milioni 35 kama ambavyo yeye mwenyewe amekuwa akisema, sasa TUCTA tunamuomba asawazishe na hata akitupa kima cha chini 500,000 hatutakuwa na nongwa,” alisema Mukoba.
Alisema wanaamini kwakuwa serikali ya Magufuli inakusanya mapato kwa kutumia ndoo na si pakacha kama ilivyokuwa kwenye serikali iliyopita, wafanyakazi watapata ahueni kwenye mishahara mwaka huu.
“Tumeshaanza kuona dalili nzuri kwenye serikali ya Magufuli kwasababu hata madai mengi ya walimu yameshalipwa na wale waliopanda madaraja wamepewa barua zao kwa hiyo tunamwangalia atatupa nini.”
MATARAJIO
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (Cotwu T), Mathias Mjema, alisema kwa kuwa Rais Magufuli ameshatekeleza ahadi zake nyingi basi ageukie kwenye mishahara ya wafanyakazi.
Alisema ni matarajio ya wafanyakazi kwamba atawathamini kwa kuwaongezea mishahara kama ambavyo alikuwa akiahidi kwenye mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Mjema alisema kwa masikio yake alimsikia mara nyingi Rais Magufuli akielezea kukerwa na kodi kubwa wanayokatwa wafanyakazi na mishahara kiduchu inayowafanya waishi maisha ya kubangaiza bangaiza.
“Mimi nimehudhuria mikutano yake tisa ya kampeni kwenye mikoa ya Dar es Salam, Morogoro, Shinyanga na Mwanza na nimemsikia kwa masikio yangu akiahidi neema kwa wafanyakazi, sasa chonde chonde tunaomba asituangushe," alisema Mjema.
Mwenyekiti wa chama hicho, Taifa Wilfred Lugendo, alisema kama Rais Magufuli amefanikiwa kutumbua majipu mbalimbali basi anapaswa kugeukia mishahara ya wafanyakazi ambayo nayo aliiita kuwa ni jipu lililoiva.
“Kodi kwenye mishahara na mishahara midogo nalo ni jipu, haiwezekani mtu anapokea mshahara tarehe 30 na baada ya wiki anaanza kukopa kopa mtaani," alisema Lugendo. "
Rais aliwahi kulisemea hili kwamba kutokana na hali ngumu walimu wengine wanatumia muda mwingi kufanya vijibiashara ili kupunguza makali ya maisha.
MGOGORO
Aprili mwaka 2010, Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi kuingia kwenye mgogoro mkubwa na TUCTA kiasi cha Shirikisho hilo kutomwalika kwenye sherehe za Mei Mosi za mwaka huo.
Mgeni rasmi kwenye sherehe za mwaka huo ambazo kwa kawaida huwa ni Rais, alikuwa aliyekuwa Rais wa Shirikisho hilo, Ayubu Omari.
Katibu Mkuu wa wakati huo ambaye bado yuko kwenye nafasi hiyo, Nicholaus Mgaya, ndiye aliyetamka hadharani kuwa hawaoni haja ya kumwalika kwenye sherehe hizo.
Mgogoro huo ulitokana na msimamo wa TUCTA kutaka serikali iongeze kima cha chini cha mshahara hadi kufikia Sh. 3500,000 wakati huo, jambo ambalo serikali ya Kikwete ililipinga kwa nguvu.
Msimamo wa Shirikisho hilo na kauli hiyo ya Mgaya ilionekana kumkera Kikwete ambaye naye alimrushia makombora wakati alipozungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee.
Kikwete aliwataka wafanyakazi kutoiga misimamo ya Mgaya na ndipo alipotoa mfano wa ndege aina ya Mbayuwayu ambaye alidanganywa na ndege mwenzake lakini alipochanganya na akili zake alibaini kuwa mwenzake kamdanganya.
Kikwete alikwenda mbali kwa kuwaeleza wazee hao wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa hawezi kutekeleza matakwa ya TUCTA na hata ikibidi kumnyima kura kwenye Uchaguzi wa 2010 wamnyime, hali iliyoendeleza malumbano na shirikisho hilo.
FEDHA NYINGI
Mwenyekiti wa Chama cha APPT Maendeleo, Kuga Mziray alisema kwasababu fedha nyingi zilikuwa zikipotea kwa kuwalipa wafanyakazi hewa ambao wameshabainika na kufutwa, basi kuna kila sababu ya kuwaongezea wafanyakazi mishahara.
Alisema watumishi wengi walikuwa wakitegemea kujilipa kwa semina, safari za ndani na nje ya nchi kutokana na mishahara midogo hivyo ni dhahiri wasipoongezewa mishahara wataishi maisha magumu zaidi na wengine wanaweza kukimbia kazi zao.
“Asipowaongezea mishahara anaweza kushangaa wengi wanazikimbia kazi za serikali maana walishazoea kutumbua fungu la matumizi mengineyo (OC), ambamo wanapata fedha za safari, semina, makongamano na maadhimisho,” alisema Mziray.
Alisema yeye binafsi aliamua kukimbia kazi ya serikalini mwaka 2000 akiwa mtaalamu wa kilimo kwenye Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi baada ya kuona anaendelea kuishi maisha magumu mwaka hadi mwaka.
“Nimeondoka serikalini nikiwa nalipwa 70,000 ambayo hata mafuta ya gari kwa mwezi haitoshi, sasa kwa mwendo wa sasa wataalamu wengi wasipoona nyongeza wanaweza kumkimbia kama mimi nilivyokimbia mwaka 2000,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa chama cha ADC, Said Miraji Abdalah, alisema wafanyakazi ndio walipaji wa kodi wakubwa licha ya mishahara midogo waliyo nayo tofauti na watu wa sekta zingine kama wakulima, wafugaji na wafanyabiashara.
“Ukiangalia anachopata mfugaji wa nyuki, mchoma mkaa, ama muuza mahindi ni kikubwa zaidi ya mfanyakazi, lakini kwasababu hana namna ya kukwepa,” alisema Miraji.
"Sasa huo mzigo wa kodi apunguziwe ili naye amudu kuishi maisha mazuri kama wengine.

No comments:
Post a Comment