Friday, 13 May 2016

Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza uwanja wa ndege wa mwl.Nyerere na kubaini dosari katika kitengo cha ukaguzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminal One) Jijini Dar es salaam.




Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei,2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.
 
Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo,walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja.
 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!