MTU aliyeshiriki Mapinduzi ya Zanzibar akikadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, Machano Mjomba Machano amezungumza na gazeti hili kuhusu siri ya umri wake na alivyoshiriki kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika 1964.
Mzee huyu ambaye familia yake inamkadiria kuwa na umri wa zaidi ya miaka 124, anaishi Gamba Mabatini, kilometa 25 kutoka Bandari ya Unguja, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, Machano ambaye anamshukuru Mungu kwa umri alionao, alisema alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika kumlinda Rais Sheikh Abeid Amani Karume wakati alipotangaza mapinduzi hayo redioni , eneo la Rahaleo.
Pamoja na masuala mengine, alisema walifanikisha mapinduzi hayo kutokana na kushikamana na kuwa na usiri mkubwa. Aidha alisema kwamba John Okello; aliyekuwa raia wa Uganda, alitumika kuwapa mafunzo ya kazi.
Mzee Machano ambaye ameona vizazi vingi vilivyokuja na kupita, inaelezwa kuwa hakuna mtu anayejua umri wake kwa usahihi. Hata yeye anasema aliambiwa umri wake wa takribani miaka 70, wakati wa mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Mtoto wake wa pili kuzaliwa kutoka mwisho, Musa Machano Mjomba ambaye ni mwalimu, alisema wanamkadiria baba yao kuwa na umri wa zaidi miaka 124. Mtoto wake wa nne kuzaliwa kati ya watoto 13 aliojaliwa, ana umri wa miaka 80 .
Ni nini sifa ya kuishi na kuona uzee mwema kama maandiko matakatifu yanavyosema? Soma makala ukurasa wa 15, Mzee Machano akieleza siri ya umri wake na nafasi yake katika Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment