Hasheem Thabeet alizaliwa februari 16 mwaka 1987 jijini Dar es Salaam.
Alianza kucheza mpira wa kikapu katika shule ya sekondari ya Makongo na kufanikiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya Makongo walioenda jijini Nairobi Kenya kushiriki kwenye mashindano ya michezo ya Afrika Mashariki.
Huko ndiko kipaji chake kilipogunduliwa na wakala mmoja wa mchezo huo ambaye aliamua kumpa schorlaship kwenye shule ya mpira wa kikapu ya Marekani.
Thabeet alienda Marekani na kujiunga na chuo kikuu cha University of Connecticut (Uconn) kuanzia mwaka 2006 hadi 2009 na kufanikiwa kuwa mchezaji tegemezi wa Uconn.
Thabeet aliisaidia Uconn kuingia kwenye timu nne za mwisho kwa mara ya kwanza tangia mwaka 2004.
Kutokana na mafaniko makubwa aliyopata Thabeet aliamua kujaribu bahati yake kwenye NBA na kuingia kwenye 2009 NBA na hatimaye kunyakuliwa na timu ya Memphis Grizzlies.
Tunampongeza na kumtakia mafanikio tele Hasheem Thabeet balozi wetu katika NBA. |
No comments:
Post a Comment