Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Chazi Mkumbo, alithibitisha mtuhumiwa huyo kuwa alikamatiwa jijini Dar es Salaam juzi na kusafirishwa hadi mkoani hapa ili kujibu shtaka linalomkabili.
Alifafanuwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kupitia hati ya mashtaka namba AR/RB/128/2013 Na AR/RB 124/2013 kwa kosa la kugushi.
Alisema polisi walifanya jitihada za kumpigia simu na kumtaka kufika mkoani hapa, lakini alikuwa akikaidi wito huo.
Alisema mtuhumiwa ambaye yupo nje kwa dhamana bado anaendelea kuhojiwa na upelezi utakapo kamilika hatafikishwa mahakamani.
Mapema mlalamikaji katika tukio hilo, Haround Emmanuel Mathayo Mlay (70) mkazi wa Sokoni one jijini hapa, alisema mtuhumiwa ambaye ni shemeji yake alimpatia hati ya nyumba yake mwaka 2004 kwa lengo la kupata mkopo wa Sh. milioni 20 kutoka benki moja jijini hapa.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alifanikisha kupata mkopo huo na kukamilisha marejesho mwaka 2008.
Alisema mwaka 2013 alishangaa kuona benki nyingine tofauti na ya awali wakija kuuza nyumba yake kwa madai kuwa nyumba hiyo imetumika kama dhamana ya mkopo ya Sh. milioni 100.
“Niliamua kuchukua hatua ya kufuatilia katika benki hiyo ndipo nilipo gundua kuna barua ya maombi ya mkopo inaonyesha niameandika mimi hata hivyo, sahihi zilizopo hapo ilionyesha jina langu na mke wangu ambaye ni marehemu zimegushiwa bila mimi kujua,” alisema.
Alisema alianza kufanya jitihada za kumtafuta mtuhumiwa wake bila mafanikio hadi kufikia mwaka jana alipo pata taarifa kuwa mtuhumiwa wake amehamishia biashara zake jijini Dar es Salaam.
“Niliendelea kumtafuta hadi nilipobaini sehemu alipokuwa akifanyia biashara zake na ndipo nilipotoa taarifa polisi na kupewa askari polisi wawili ambao juzi walifanikiwa kumkamata na kumrejesha jijini Arusha,’’ alisema.
NIPASHE

No comments:
Post a Comment