Watu wanne waliofahamika kuwa ni majambazi wameuwawa katika eneo la mapango ya Amboni wakati wa majibizano ya risasi yaliokuwa yakifanywa na askari wa jeshi la polisi na majambazi hao ambao walikuwa wameweka kambi katika mapango hayo yaliopo mjini Tanga.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Tanga Leonard Paulo amethibitisha hayo leo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu matukio ya ujambazi yaliokuwa yakijitokeza mara kwa mara na kugharimu maisha ya wananchi.
Kamanda Leonard Amesema mbali na jeshi la polisi kufanikiwa kuwadhibiti majambazi hao pia jeshi hilo limefanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vinavyosadikika kuwa vilikuwa vinatumika katika kufanyia matukio ya ujambazi.
Amevitaja vifaa vilivyo kamatwa kuwa ni vocha mbalimbali za simu 195, majambia 7, mapanga 4, msumeno mmoja, risasi 17 za bunduki aina ya short gun, sare za mgambo, Kofia inayofanana na sare za jeshi la wananchi wa Tanzania, na pikipiki 2
Amesema wakati wakiendelea na uchunguzi watu 4 wamekamatwa ambao ni majambazi na waliwataja majambazi wenzao ambao waliweka kambi katika mapango ya ambano ndipo jeshi likavamia eneo hilo na kufanikiwa kuwauwa majambazi 4 na mmoja kujeruhiwa.
Kamanda amewataja majambazi hao waliuwawa wakati wa mapambano kati ya askari polisi na majambazi hao kuwa ni Nasibu Bakari,Abuu Katada,Abuu Mussa pamoja na raia wa kigeni alietambulika kwa jina la Idrisa Berato.
Katika majibizano ya risasi baina ya majambazi na askari wa jeshi la polisi askari polisi 2 wamejeruhiwa ambao ni Gwantwa Mwakisole, mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi mkoani Tanga na PC Charles ambao walikuwepo katika mapambano hayo na kwamba wamepatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment