Jeshi la Misri na shirika la safari za ndege nchini humo zimesema kuwa mabaki ya ndege ya Egyptair iliotoweka yamepatikana katika bahari ya Mediterenean.
Ndege hiyo aina ya Flight 804 ilikuwa ikielekea kutoka Paris kuelekea Cairo ikiwa na abiria 66 na wafanyikazi wakati ilipotoweka siku ya Alhamisi.
Msemaji wa jeshi la Misri alisema kuwa mabaki na abiria wa ndege hiyo walipatikana kilomita 290 kutoka mji wa Alexandria.
Katika taarifa yake ,rais Abdel Fattah al-Sisi alisikitishwa na ajali hiyo.
Kampuni ya ndege ya EgyptAir pia ilithibitisha kupatikana kwa mabaki hayo katika mtandao wake wa Twitter.
Mataifa ya Ugiriki,Misri,Ufaransa na Jeshi la Uingereza yamekuwa yakishiriki katika oparesheni ya kuisaka ndege hiyo karibu na kisiwa cha Karpathos.
Ugiriki inasema kuwa rada yake imekuwa ikionyesha kwamba ndege hiyo iligeuka kwa ghafla mara mbili na kuanguka kutoka futi 25,000 na kuingia katika maji.
No comments:
Post a Comment